
Kocha
wa timu ya taifa ya Louis van Gaal amesema kuna uwezekano wa kumuanzisha
mshambuliaji wa wake Klass-Jan Huntelaar badala ya Robin van Persie kwenye mchezo wa
Ijumaa dhidi ya Andorra.
Akizungumza na Mtandao wa Soccerway, Van Gal amesema anatazamia kufanya hivyo kulingana na ubora wa wachezaji hao na nafasi wanazocheza uwanjani ikiwa wote wanasimama kama washambuliaji wa kati.
Aliongeza kuwa anafahamu uwezo wa mshambuliaji wa Manchester
united Robin Van Parse sambamba na
Huntelaar anayechezea Sharke 04 ya
ujerumani, ila Van Parse atakuwa na wakati mgumu kuanza kwenye mchezo huo.
Van Gal anaingia alianza kuifundisha Uholanzi Julai 6 mwaka
huu, baada ya kufutwa kazi aliekuwa kocha wa timu hiyo Bert Van Marwjik, wakati sasa anakibarua kigumu cha kutafuta tiketi ya kombe la dunia mwaka 2014 kule nchini Brazil.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment