Sekretarieti ya chama cha waandishi wa habari
za michezo TASWA imefikia hatua ya mwisho ya mazungumzo na mdhamini wa Mkutano
Mkuu wa chama hicho, unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao katika tarehe ambayo
itatangazwa rasmi.
Kamati ya Utendaji ya TASWA ilikubaliana
katika kikao chake mwezi uliopita kuwa Mkutano Mkuu wa TASWA mwaka huu uwe wa
aina yake kwa kuwawezesha wanachama kukaa pamoja na kubadilishana mawazo huku
ikashauri mkutano huo ufanyike nje ya Dar es Salaam kama hali itaruhusu.
Akizungumzia hilo katibu mkuu wa Taswa Amiri
Muhando, amesema tayari suala la kutafuta mdhamini limefanyika na mdhamini
amepatikana, na wapo kwenye hatua ya mwisho ya mazungumzo kabla ya kutajwa
mapema wiki ijayo .
Kwa
upande mwingine Muhando amewaka wanachama ambao hawajalipa ada zao wafanye
hivyo kwa kuwasiliana na Mhazini wa chama au Mhazini Msaidizi ili waepuke
usumbufu wa kushindwa kuhudhuria mkutano huo
0 comments:
Post a Comment