
Kim Poulsen
Kocha Mkuu wa timu ya soka ya
Tanzania(Taifa Stars), Kim Poulsen mwishoni mwa wiki hii ataanza ziara wisiwani
Zanzibar kuangalia Ligi Kuu ya nchini humo.
Kim anatarajia kushuhudia takribani
mechi tano akianzia kisiwani Pemba ambapo kati ya Oktoba 19 na 21 atashuhudia
mechi mbili zitakazochezwa kwenye Uwanja wa Gombani. Mechi hizo ni kati ya
mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Super Falcon watakao cheza na vinara wa ligi
hiyo Bandari, na baadaye mechi kati ya timu ya Duma na Bandari.
Baadaye atakwenda Unguja kwenye
Uwanja wa Amaan ambapo baadhi ya mechi alizopanga kushuhudia ni kati ya Mtende
na Chipukizi, Mundu na Jamhuri na KMKM dhidi ya Zimamoto.
Ziara ni moja ya mikakati mikubwa ya
kuhakikisha anapata kikosi bora cha timu ya taifa ya Tanzania.
0 comments:
Post a Comment