
Uwanjwa wa Anfield.
Klabu ya Liverpool, imetangaza mpango wake wa kuboresha uwanja wake wa Anfield wanao utumia michezo
mbalimbali na kuacha mpango wa kujenga
uwanja wa mpya wa timu hiyo.
Mkurugenzi wa Liverpool, Ian Ayre, amethibitisha kuwa uwanja huo
utaboreshwa kutoka mashabiki 45,276 hadi
60,000 na upanuzi huo wa uwanja
utagharimu kiasi cha paundi milioni 150.
Amesema uongozi wa Liverpool, umelipa kiasi cha paundi milion 25
kama kodi ya kupata eneo la kutanua uwanja huo, wakati mchoro kamili wa ujenzi
huo utawekwa wazi rasmi mwezi ujao huku mpango wa ujenzi rasmi kuanza kazi
majira ya kiangazi mwakani.
Mpango huo utajumuisha mitaa kadhaa ambayo itaingizwa katika eneo
la uwanja ikiwemo mitaa, Lother,Alroy na Sybil huku maeneo yatakayofanyiwa
maboresho makubwa ni eneo la jukwaa kuu na maeneo baadhi ya maeneo ya muhumi ya klabu hiyo.
Chanzo na BBC.
0 comments:
Post a Comment