YANGA YADAI KUFUNGWA KIHALALI.



 
                      Katibu wa Yanga, Mwalusako
Baada ya kupokea kichapo kwenye mchezo wa ligi hapo jana dhidi ya Kagera Sugar uongozi wa labu ya Yanga umesema timu yao ilifungwa kimchezo na si kwa sababu nyinginezo.

Hayo yamesemwa hii leo na katibu wa Yanga Lawrence Mwalusako kuwa sababu zilizosambazwa kuwa walifikia hoteli mbovu na chakula kibovu, ndio sababu ya kufungwa siya kweli.

Mwalusako amekanusha habari zilizoandikwa na gazeti moja la leo, kwamba wachezaji wake walilala wawili wawili kitanda kimoja mjini Bukoba.

Kuhusu michezo inayofuata Mwalusako amesema kwa sasa wanatafuta mbinu nzuri za kupata ushindi nje ya Dar es Salaam ambayo imekuwa kikwazo kwa kiasi kikubwa.

0 comments:

Post a Comment