EDGA APATA ULAJI NCHINI ENGLAND.



 
               Edga Davies enzi zake akiwa na Uholanzi.
Kiungo wa zamani wa timu ya taifa Uholanzi Edger Davis amepata nafasi ya kuwa kocha mchezaji  wa klabu ya Barnet inayoshiriki ligi daraja la pili ya nchini England.
Davis ambaye katika maisha yake ya soka amewahi kuvichezea vilabu vya Ajax Amsterdan,Juventus na Fc Barcelona ametangaza kupitia ukurasa wake wa Twita akisema nayofuraha  kwa kujiunga na timu yake ya zamani kwakuwa kocha mchezaji.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 39 atakuwa akishirikiana na kocha mkuu wa timu ya Barnet  Mark Robson  taarifa zilizothibitishwa na mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo Paul Fairclough.
Vilabu vingine alivyowahi kuvichezea nyota huyo ni Inter Milan,Tottenharm  pamoja na Crytal Palace  ambapo hadi sasa amecheza mechi 412 na kufunga magoli 32.
Taarifa toka Soccerway.

0 comments:

Post a Comment