MUDIFA YAOMBA TIMU ZIJIANDAE.



Uongozi wa chama cha soka wilaya ya Mufindi MUDIFA umevitaka vilabu vya wilaya hiyo kujiandaa kwa ligi ya wilaya wakati wakisubiri maelezo ya mfumo  mpya wa ligi za wilaya toka katika shirikisho la soka nchini TFF.
Katibu mkuu wa MUDIFA, Festor Kilipamwambu alizungumza hayo Sambamba na kuwataka watendaji wa kata takribani zote za wilayani Mufindi kuandaa viwanja kwaajili ya kuchezewa michezo ya ligi hiyo iliyoshindikana kuanza mwezi huu.
Kilipamwambu amesema kata zinatakiwa kuandaa viwanja ili kutimiza hazma ya kuchezwa ligi kwa mtindo wa nyumbani na ugenini sambamba na kukuza mchezo wa soka wilayani humo.
Kabla ya kuanza kwa ligi ya wilaya tayari timu za Mucoba FC, Ifwagi, JKT Mafinga na Changarawe zimeshafuzu kucheza ligi ya mkoa kutokana na mabadiliko ya mfumo katika uendeshaji wa ligi za Tanzania bara.

0 comments:

Post a Comment