Timu ya Njombe mji, toka mkoa mpya wa Njombe siku ya jumapili
itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Majimaji ya songea kwenye uwanja
wa Amani, Mjini Makambako.
Akizungumzia mchezo huo, katibu mkuu wa Njombe Mji, Obeid
Mwakasungura amesema mchezo huo ni maandalizi tosha ya ligi ya wilaya kwa mwaka
huu.
Amesema tayari mpaka sasa timu hiyo imezidi kuimarika
kufuatia michezo waliocheza dhidi ya Mbeya City na Serengeti Boys, ambayo yote
walimaliza kwa kufungwa.
Msimu uliopita Njombe mji, ilishindwa kufanya vyema kwenye
hatua ya mwisho ya ligi mkoa kutokana na kushindwa kumudu mikiki ya upinzani
uliokuwemo toka kwa timu nyingine za mkoa wa Iringa ikiwemo Kurugenzi.
0 comments:
Post a Comment