
Mwenyekiti wa chama cha wachezaji wa kulipwa nchini
England PFA, Clarke Carlisle amesema kuwa adhabu aliyopewa mlinzi wa Chelsea
Jonh Terry kwa kusimamishwa michezo minne haikutosha kama adhabu ya mchezaji
huyo.
Carlisle
ambaye kwa sasa anacheza klabu ya York City ya nchini humo, amesema kuwa
angalia adhabu ya Suarez iliyotolewa 20
Decemba 2011, kwa kosa la u
ubaguzi dhidi ya Patrice Evra alitozwa
michezo minane na faini ya paundi 40000 huku akipewa kiasi cha siku 14 za
kukata rufaa.
Lakini Terry
amefungiwa michezo minne na faini 220000 huku akipewa siku 18 za kukata rufaa
yake.
Carlisle
amitaka kamati ya nidhamu ya FA kuwa kuongeza adhabu kwa terry na kumfanya achangie katika kampeni
dhidi ya ubaguzi wa rangi.
0 comments:
Post a Comment