
Msemaji wa Simba E.Kamwaga
Uongozi wa klabu ya Simba umevitaka vyombo vya habari kusema
uongo juu ya klabu yao haswa kuhusu wachezaji wa klabu hiyo,
Hayo yamesemwa na msemaji wa timu hiyo Ezekiel Kamwaga mchana
wa leo wakati akizungumza kuhusu uzushi wa kusimamishwa kwa Mrisho Ngasa juu ya
kucheza chini ya Kiwango dhidi ya Yanga siku ya jumatano.
Kamwaga amesema kuwa
hakuna maamuzi kama hayo ndani ya Simba na sababu ya Ngasa kucheza chini ya
Kiwango imetokana na kusumbuliwa na ungonjwa wa Maralia. Huku akithibitisha
kuwa nyota huyo hatokuwemo kwenye kikosi cha kesho kitakacho cheza na JKT
Orjoro.
Aliongeza kuwa si Ngasa pekee atakae kosa mchezo ila mlinzi mahiri wa timu hiyo
Shomary Kapombe anaeumwa bega na mguu pamoja na Shamte Haruna alieumia akiwa
mazoezini visiwani Zanzibar.
Kwa upande wa malalamiko ya Mapato katika mchezo wake dhidi
ya Yanga Kamwaga amesema kwa upande wao hawakuona mapungufu na kuwataka wadau
wajitokeze katika michezo ili kuongeza kipato zaidi , ila amevitaka vilabu
vyote kuwa na miradi yenye kuchangia maendeleo ya vilabu hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment