Ritta Kabati
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia tiketi ya chama cha mapindui mheshimiwa
Ritta Kabati hapo jana amekabidhi kiasi
cha shilingi laki mbili kwa chama cha mpira wa kikapu mkoani Iringa ambayo kwa
sasa inaiandaa timu ya mkoa inayotarajiwa kushiriki michuano ya taifa Cup itakayofanyika jijini Tanga mwezi huu.
Akizungumza
na Twalib Omary mara baada ya kutoa pesa hizo Kabati amesema kuwa hiyo ilikuwa ni
sehemu ya ahadi aliyotoka katika kipindi chote cha mapumziko ya vikao vya bunge
na anatambua umuhimu wa michezo sambamba na mchezo huo wa kikapu ambao
umepoteza njia mkoani Iringa.
Aliongeza
kwa kuwataka wadau kujitokeza vya kutosha katika kuisaidi michezo ili kupata
timu mahiri zitakazo tuwakilisha katika mashindano mbalimbali hapa nchini,
Kwa upande wake katibu mkuu wa muda wa chama
cha kikapu mkoani iringa IRBF, Jamal Asedi ameshukuru kupokea kiasi hicho na
kuwataka wadau wajitokeze kutoa zaidi ili kuhakikisha timu inasafiri, lakini
pia amefanunua kuwa michuano hiyo kwa sasa itaanza rasmi Oktoba 29 mwaka huu
baada ya 18 iliyopangwa hapo awali.
0 comments:
Post a Comment