TIMU ZA AFCON 2013 ZAPATIKANA.



       
 Beki wa Zambia Sunzu akishangilia ubingwa wa Afrika 2012
Shirikisho la soka barani Afrika Caf limekamilisha droo ya timu shiriki za michuano mataifa ya Africa kwa mwaka 2013 baada ya kumalizika kwa michezo ya kufuzu mwishoni mwa wiki iliyopita.
Timu zilizofuzu michuano hiyo ikwemo timu ya Ethiopia ambayo iliwahi kutwaa taji hilo mwaka 1962 na kushiriki michuano hiyo kwa mara ya mwisho mwaka 1982 kabla kupata tena nafasi hiyo mwaka huu.
Ivory Coast imeingizwa kwenye orodha ya timu hizo mbali na mchezo wake dhidi ya Senegal kuvunjwa kutokana na vurugu za mashabiki wa Senega waliojitokeza nchini Dakar
Timu zilizofuzu ni Algeria, Angola, Burkina Faso, Ivory Coast, DR Congo, Ethiopia, Ghana, Cape Verde, Mali, Morocco, Niger, Nigeria, Togo, Tunisia pamoja na Zambia na
Makundi ya michuano hiyo yatatangazwa oktoba 24 mwaka huu kule mjini Durban wakati michuano yenyewe itaanza rasmi january 19 hadi february 10 mwakani.

0 comments:

Post a Comment