MISRI YAINGIA MITINI.



            
                        Kikosi cha Serengeti Boys
Timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) imefuzu kucheza raundi ya tatu na ya mwisho kwenye michuano ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Vijana baada ya Misri kujitoa.

Akithibitisha hilo msemaji wa TFF, Boniface Wambura amesema Serengeti Boys ilikuwa icheze raundi ya pili dhidi ya Misri Oktoba 14 mwaka huu jijini Dar es Salaamkabla ya kurudiana baada wiki mbili lakini imeshindikana kutokana na kutokamilika kwa maandalizi ya timu ya Misri.

Amesema Serengeti Boys  itacheza raundi ya tatu kwa kumkabili mshindi wa mechi kati ya Zimbabwe na Congo Brazzaville. Mechi ya kwanza itachezwa Novemba 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati ya marudiano itafanyika ugenini wiki mbili baadaye.

Katika raundi ya kwanza Serengeti Boys inayofundishwa na Jakob Michelsen kutoka Denmark ilikuwa icheze na Kenya mwezi uliopita, lakini nchi hiyo ilijitoa katika michuano hiyo ambayo fainali zake zitachezwa Machi mwakani nchini Morocco.

Zimbabwe na Congo Brazzaville zitapambana zitapambana kati ya Oktoba 12-14 mwaka huu, Zimbabwe ikiwa mwenyeji wa mechi ya kwanza wakati ya marudiano itafanyika kati ya Oktoba 26-28 mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment