
Baada ya kufungiwa kwa muda wa miezi kumi kocha wa timu ya Juventus Antonie Conte hii leo kocha huyo amepunguziwa adhabu hadi kufikia miezi minne.
Maamuzi hayo yametolewa na kamati ya Olimpic ya nchini Italia ambayo Conte alipeleka rufaa yake kusikilizwa na kutolewa maamuzi hayo ambayo yamemfanya Conte kurudi uwanja kama kocha wa Juve Desemba 9 mwaka huu.
Katika adhabu ya kwanza Conte alitakiwa kurejea uwanjani Juni 9 mwaka 2013katika hicho ambacho kwa sasa kinaongozwa na mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo Massimo Carrera.
Conte ni nyota wa wazamani wa Juventus mwenye umri wa miaka 43 huku akiwa na rekodi ya kucheza michez 400 kwenye klabu hiyo sambamba na kutwaa ubingwa Serea A msimu wa 2011-2012 bila ya kufungwa mchezo hata mmoja.
0 comments:
Post a Comment