MCHUNGAJI MSIGWA KUDHAMINI LIGI YA WILAYA



 
Mbunge wa jimbo la IringaMjini  kupitia tiketi ya Chadema, Mchungaji Piter Msingwa, yupo katika mikakati ya kudhamini ligi ya wilaya ya Iringa mjini kwa msimu wa mwaka 2012.
Akizungumza na Mwananchi mratibu wa michezo katika ofisi ya mbunge huyo Abu Changawa amesema kuwa udhamini huo utazingatia uandaaji wa timu zitakazo shirki katika ligi wilaya hiyo, kwa kutoa vifaa vya michezo ikiwemo jezi na mipira sambamba na posho kwa waamuzi wa michezo ya ligi hiyo.
Aliongeza kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha soka la Iringa linarejea katika heshima yake iliyopotea takribani miaka 11 iliyopita.
Majeki amesema,Mh Msigwa bado yupo katika  harakati za mwisho ili kufaninikisha zoezi hilo linalotaka kufanyika kwa mkataba wa mwaka mmoja kati yak e na chama cha soka wilaya IMDFA.
Msimu uliomalizika wa mwaka 2011 mbunge huyo aliahidi kutoa zawadi kwa mshindi wa kwanza wa ligi hiyo ambaye ni Magorofani hatimaye hakuitekeleza ahadi ya zawadi ya jezi.
Lakini pia ahadi hiyo ilitolewa na Meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi na katibu wa soka Iringa Eliud Mvela lakini hawakutekeleza zawadi hizo za washindi wa ligi ya wilaya Iringa
Wakati huohuo katibu msaidizi wa chama cha soka wilaya ya Iringa mjini, Rashidi Ali Shungu, amesema ligi ya wilaya hiyo itaanza tarehe 10 oktoba na ratiba itatolewa oktoba saba mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment