
Benito Malangalila katikati akiwa na katika harakati za Muungano cup
Mazishi ya aliekuwa mbunge wa jimbo la
Mufindi Kusini muheshimiwa Benito Malangalila yaliyopangwa kufanyika leo
yamesogezwa mbele hadi hapo kesho saa 6 kamili mchana.
Akizungumza nasi mratibuwa michuano ya
Muungano na mjumbe wa soka la vijana TFF amesema kuwa mazishi ya mwenyekiti
huyo wa kamati ya Muungano
yameshindikana kufanyika hivi leo kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya maandalizi
ya mazishi hayo.
Lakini mbali na hayo amethibitisha kuwa
mpaka itakapofika usiku wa hii leo kila
kitu kitakuwa kimekwenda sawa kwa upande wa maandalizi.
Yasini amesema mpaka leo hii wadau na
viongozi mbalimbali wamekuwa wakituma salamu za rambirambi kwa familia ya
marehemu Malangalila iliyopo Changarawe mjini Mafinga.
Mung u aiweke roho ya Marehemu Malangalila mahala pema
peponi Amen.
0 comments:
Post a Comment