Kamisheni ya Ngumi za
Kulipwa Nchini (TPBC) inachukua fursa hii kumuenzi baba wa taifa “Mwalimu Julius Kambarage Nyerere” wakati
Tanzania inaadhimisha miaka 13 ya kifo chake. Juhudi za mwalimu katika kuleta
maendeleo ya michezo pamoja na haki, usawa na ushirikiano kwa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania tutazienzi daima.
TPBC inakumbuka na kuenzi
mchango wa baba wa taifa katika tasnia ya michezo hususan ngumi za kulipwa
nchini tukikumbuka kuwa ni miaka ya mwisho ya utawala wake ndipo ngumi za kulipwa
zilianza rasmi Tanzania mwaka 1982.
Juhudi za baba wa taifa
za kuendeleza michezo zilikuwa na sura mbili kubwa:
Sura ya kitaifa: Michezo wakati wa utawala wa baba wa
taifa ilianzia kwenye shule za msingi na kwenye vitongoji na hivyo kuwapa nafasi
nzuri watanzania wengi wakati mzuri sana wa kushiriki na kuchangia kwenye maendeleo
ya michezo.
Hii ilisaidia watanzania
kujenga ari na vipani vya michezo ambavyo huanzia kwenye umri mdogo na hivyo
kushiriki kwao kwenye michezo kuanzia shule za msingi na vitongoji kuliwapa nafasi
nzuri ya kujijenga kimichezo.
Umri mzuri unaotakiwa
kuanza kujishughulisha kwenye michezo ni kuanzia miaka 7 na kuendelea. Mtu anapoanza
kujishughulisha kwenye michezo mapema akiwa na umri mdogo huweza kuonyesha na
kuendeleza kipaji chake mapema na kwa hali ya juu.
Baba wa taifa
alijenga msingi wa umoja na usawa ambao uliwezesha watanzania wote kushiriki katika
michezo bila ubaguzi wa ukabila, udini na jinsia jambo ambalo halikuwa rahisi
kwa nchi nyingine wakati ule.
Sisi tumejionea miaka
ya karibuni kwenye michezo ya Olimpiki iliyomalizika katika jiji la London,
Uingereza baadhi ya wanamichezo wa jinsia moja ndipo waporuhusiwa.
Hivyo baba wa taifa
aliwezesha watanzania wote kushiriki kwenye michezo bila ubaguzi.
Sura ya Kimataifa: Serikali ya baba wa
taifa ilijenga msingi imara kwa vyama vya kitaifa vya Tanzania kujiunga kwenye
na mashirikisho mengi ya kimataifa kama vile CECAFA, Olimpiki, FIFA, AIAA, IBF,
WBC, WTA na mengine mengi.
Uanachama huu watanzania
kwenye mashirikisho haya uliweza kujenga misingi ya “Utalii wa Michezo” kwa Tanzania kujulikana duniani na hivyo
kuwezesha nchi kutangaza vivutio vyake vya utalii na mahala pazuri pa kuwekeza.
Ni wakati wa utawala
wa baba wa taifa mchezo wa riadha uliweza kuitangaza sana Tanzania katika
medani ya kimataifa.
Jambo hili halina
budi kuigwa na kuendelezwa na awamu zilizomfuata mwalimu hususan awamu ya sasa.
Sisi tunafikiri kuwa
wakati rais wa sasa wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kiongozi
wa kwanza mbali na mwalimu kuwekeza juhudi zake binafsi katika kuendeleza
michezo, wale waliopewa jukumu la kusimamia tasnia hii hawana budi kumsaidia
kuzifanya juhudi hizi zizae matunda.
Tunachukua fursa hii
adimu ya kumuenzi baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika juhudi
zake za kuendeleza michezo katika jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais: Onesmo Alfred
McBride Ngowi
Makamu
wa Rais:
Godfrey Madaraka Nyerere
Katibu
Mkuu:
Nemes Kavieshe
Katibu
Mkuu Msaidizi:
Nicholus Mallya
Mwenyekiti
wa Viwango na Ubingwa: Boniface Wambura
Wajumbe
wa Kamati ya Utendaji: Mark Hatia, Henry Mfinanga, Michael Buchato,
Imetolewa
na Uongizi:
Onesmo Alfred McBride Ngowi
Rais,
Kamisheni ya Ngumi za
Kulipwa Nchini (TPBC)
0 comments:
Post a Comment