Baada
promota maarufu wa ngumi za kulipwa kutoka nchini Misri Richard Nwoba wa
kampuni ya “Louaa Boxing Promotions”
kuzitembelea ofisi za IBF zilizoko jijini Dar-Es-Salaam ili kuona namna
ya kupromoti mapambano ya ngumi katika ukanda wa Mashariki ya Kati.
Rais
wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi “Onesmo Ngowi katika ziara hiyo ya Nwoba
wamefikia makubaliano ya kushirikiana na makampuni matatu ya Tanzania
kupromoti mapambano manne ya ubingwa wa IBF katika mwezi wa Novemba.
Katika
makubaliano hayo mabondia kadhaa wa Tanzania, Kenya na Misri watapambana
kuwania mataji manne ya IBF Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba za Uarabu na
Uajemi. huku ikiwa faraja kwa bondia Francis
Cheka wa Tanzania ambaye atachuana bondia toka nchini Oman, Amin Saad Mabrook katika mpambano
utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu.
Richard
Nwoba ni bondia wa zamani na makao yake makuu yako katika jiji la Cairo nchni
Misri ambako anaendesha biashara ya ulinzi wa makampuni pamoja na kupromoti
ngumi za kulipwa akiendesha kampuni ya
“Louaa Boxing Promotions.
MWISH
0 comments:
Post a Comment