1.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF katika kikao chake kilichofanyika tarehe 03-04 Oktoba
2012 ilijadili michakato ya chaguzi za vyama vya mpira wa miguu vya Mikoa ya
Rukwa (RUREFA), Arusha (ARFA), Shinyanga (SHIREFA), Pwani (COREFA), Dar es
Salaam (DRFA) na Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT). Kamati
iliamua yafuatayo:
(a)
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Arusha (ARFA)
Uchaguzi wa ARFA utafanyika
Jumapili, tarehe 07 Oktoba 2012 mjini Arusha kama ulivyopangwa.
(b)
Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT)
Uchaguzi wa FRAT utafanyika Jumapili,
tarehe 07 Oktoba 2012 mjini Dodoma kama ulivyopangwa.
(c)
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA)
Uchaguzi wa COREFA utafanyika
Jumapili, tarehe 14 Oktoba 2012 Wilayani Mafia kama ulivyopangwa.
(d)
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA)
Kamati ilibaini na
kujiridhisha kuwa kulikuwa na udanganyifu uliofanywa na Kamati ya Utendaji ya
RUREFA katika kutekeleza majukumu yake ya kikatiba hususan, uteuzi wa baadhi
ya wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA. Pamoja udanganyifu huo,
Kamati ya Uchaguzi ya TFF imejiridhisha kuwa Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA
imeshindwa kutimiza wajibu wake katika kusimamia uchaguzi wa RUREFA, hata baada
ya kuwa imepewa onyo kuzingatia matakwa ya Kanuni za Uchaguzi.
Kutokana na udanganyifu
uliofanyika katika uteuzi wa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA,
Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa mujibu wa Kanuni
za Uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 26(2) na (3) na Katiba ya TFF Ibara ya
49(1), imeamua yafuatayo:
(i) Imeifuta Kamati ya Uchaguzi
ya RUREFA. TFF itateua Kamati mpya ya Uchaguzi ya RUREFA itakayoandaa na
kusimamia uchaguzi wa RUREFA.
(ii)Uteuzi wa Kamati mpya ya Uchaguzi
ya RUREFA utafanyika wakati muafaka baada ya TFF kukamilisha taratibu za
uteuzi, na ratiba ya uchaguzi ya RUREFA itatangazwa baada ya zoezi hilo.
(e)
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA)
Kamati ya Uchaguzi ya TFF
imebaini kuwa baadhi ya viongozi wa Kamati ya Utendaji ya SHIREFA wanaingilia
mchakato wa uchaguzi wa SHIREFA kinyume na matakwa ya Kanuni za Uchaguzi
za wanachama wa TFF. TFF haitambui maamuzi ya uongozi wa SHIREFA wa kuivunja Kamati
ya Uchaguzi ya SHIREFA inayosimamia uchaguzi wa Chama hicho. Zoezi la uchaguzi
wa SHIREFA lililoanza tarehe 08 Septemba 2012 linaendelea na uchaguzi wa
viongozi wa SHIREFA utafanyika tarehe 20 Oktoba 2012 kama ulivyopangwa.
(f)
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA)
Kamati ya Uchaguzi ya TFF
itakamilisha zoezi la kusikiliza rufaa zilizokatwa dhidi ya maamuzi ya Kamati
ya Uchaguzi ya DRFA na kupitia mchakato mzima wa uchaguzi wa DRFA, ili
kujiridhisha kama matakwa ya Katiba ya DRFA na TFF yamezingatiwa. Kamati ya
Uchaguzi itatoa uamuzi kuhusu rufaa zilizowasilishwa kwenye Kamati kwa mujibu
wa Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF na kuhusu mchakato wa uchaguzi wa
DRFA baada ya kikao chake kitakachofanyika Jumanne, tarehe 09 Oktoba 2012.
2.
Kuzingatia Kanuni za Uchaguzi:
(i) Kamati ya Uchaguzi ya TFF
itaishauri Mamlaka husika ya TFF kuwachukulia hatua za kinidhamu viongozi wa
Kamati za Utendaji walioko madarakani wanaoingilia michakato ya chaguzi za
wanachama wa TFF na kusababisha mikanganyiko katika chaguzi ili ama wandelee
kuwa madarakani kinyume na matakwa ya Katiba ya TFF Ibara ya 12(2)(a) au
wapitishwe kugombea uongozi kinyume na taratibu zilizowekwa na TFF.
(ii)Kamati ya Uchaguzi ya
TFF inasisitiza na kuzitaka Kamati za Uchaguzi za vyama wanachama wa TFF
kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF wakati wote wa michakato ya
uchaguzi wa viongozi wa vyama hivyo.
SERENGETI BOYS KUVUNJA KAMBI KWA MECHI
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri
chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) ambayo imepata tiketi ya kucheza raundi ya
tatu ya michuano ya Afrika baada ya Misri kujitoa itavunja kambi yake kwa mechi
ya kirafiki dhidi ya kikosi cha Yanga cha U20.
Mechi hiyo itachezwa kesho (Oktoba 6
mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30
jioni. Kiingilio kwenye mechi hiyo kitakuwa sh. 2,000 tu.
TAFCA YAONGEZA MUDA WA KUCHUKUA FOMU
Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Makocha
wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) imeongeza muda kwa wagombea kuchukua fomu
kwa ajili ya uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika katikati ya mwezi ujao.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya
Uchaguzi ya TAFCA, Ramadhan Mambosasa, jana ndiyo ilikuwa mwisho wa kuchukua
fomu lakini mwitikio wa wagombea umekuwa mdogo ambapo ni watano tu
waliojitokeza.
Hivyo, amesema wameongeza muda wa
kuchukua na kurudisha fomu ambapo mwisho itakuwa ni Oktoba 9 mwaka huu saa 10
kamili alasiri. Fomu zinapatikana ofisi za TAFCA ambazo ziko Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti,
Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF,
Mhazini na wajumbe watatu wa Kamati ya Utendaji.
0 comments:
Post a Comment