
Kiungo wa
timu ya taifa ya Englanda Frank Lampard ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya
taifa ya England baada ya kupata jeraha la goti wakati akiwa katika mazoezi na
timu hiyo.
Chama cha
soka cha England FA kimesema kuwa kiungo
huyo atarejea katika timu ya Chelsea kwaajili ya matibabu kabla jumapili
kujiunga tena na kikosi cha England kwajili ya mchezo dhidi ya Poland
utakaocheza siku ya jumanee.
Kutokana na hali hiyo kocha Roy
Hogson amefanya maamuzi ya kumwita mchzaji wa Liverpool,Jonjo Shelvey kwaajili kuziba nafasi hiyo na mlinzi wa
Chelsea Ryan Bertrand anaeziba nafasi ya beki wa Arsena Kieran Gibbs ambaye pia
ni majeruhi.Siku ya Ijumaa England inakabiliwa na mchezo wa kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 kule nchini Brazil dhidi ya San Marino kabla ya kuwakabili Poland siku ya Jumanne.
Wakati huo
mshambuliaji wa Manchester united, Wayne Rooney ametajwa kuwa atavaa kitambaa
katika mchezo wa Ijumaa dhidi ya San Marino utakaoshuhudiwa na washabiki
wapatao 90,000 kwenye uwanja wa Wimbley.
Roony mwenye
umri wa miaka 26 na kucheza michezo 76, anachukua nafasi hiyo badala ya nahodha
wa England na Frank Lampard kuondolewa kwenye orodha ya wachezaji watakaoshiriki siku hiyo
kutokana na majeruhi.
Kikosi cha
England cha sasa makipa ni Fraser Forster (Celtic), Joe Hart (Manchester City), John Ruddy
(Norwich) Walinzi Leighton Baines (Everton), Ryan Bertrand (Chelsea), Gary Cahill (Chelsea), Ashley Cole (Chelsea), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool), Joleon Lescott (Manchester City), Ryan Shawcross (Stoke), Kyle Walker (Tottenham)
viungo Michael Carrick (Manchester United), Tom Cleverley (Manchester United), Steven Gerrard (Liverpool), Adam Johnson (Sunderland), Aaron Lennon (Tottenham), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Jonjo Shelvey (Liverpool), Theo Walcott (Arsenal)
washambuliaji ni Andy Carroll (West Ham), Jermain Defoe (Tottenham), Wayne Rooney (Manchester United), Danny Welbeck (Manchester United)
0 comments:
Post a Comment