OWEN COYLE AVULIWA GAMBA BOLTON.



 Bolton Wanderers manager Owen Coyle
                      Aliekuwa kocha wa Bolton, Owen Coyle
Kocha wa klabu ya Bolton Wonderers, Owen Coyle amefukuzwa kazi katika klabu hiyo aliyokuwa akiifundisha tangu tangu alipojiunga nayo January 8 mwaka 2010.
Kocha huyo ambaye katika miaka ya 90, aliwahi kuchezea timu hiyo, kufutwa kwa mkataba wake kumetokana na kushinda mechi tatu kati ya kumi za ligi ya mabingwa ya nchini England huku ikiwa nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Baada ya maamuzi hayo mwenyekiti wa Bolton Wonderers, Phil Gartside, ameushukuru mchango wa Coyle na jopo lake katika kipindi chote alichokuwa na timu hiyo.
Kwa upande wake Coyle, amesema alijitahidi kufuata vile Bolton inataka tangu akiwa mchezaji lakini mambo yamekuwa magumu kwa hiyo hana budi kuwashukuru viongozi na mashabiki wa klabu hiyo.
Coyle mwenye umri wa miaka 46, aliwahi kuifundisha timu ya Burnley kwa miaka mitatu na kuipandisha ligi kuu ya England EPL kabla ya kuhama na kujiunga na  Bolton Janury 8 2010 ambayo alishuka nayo msimu wa 2011-2012.

0 comments:

Post a Comment