CARLO AMPONDA ZLATAN.



 
                         Zlatani akiwa na jezi PSG.
Baada ya sare ya jana dhidi ya Olimpic Marsele kocha wa Paris Saint-Germain Carlo Ancelotti amesema kuwa hakuvutiwa na kiwango cha mshambuliaji wake Zlatan Ibrahomovic katika mchezo huo wa saba wa Ligi one.
katika mchezo huo Zlatan alifunga magoli mawili na kusababisha matokeo hayo suluhu lakini kocha huyo wa kitaliano amesema anaujua vizuri uwezo wa Zlatan kuliko alivyofanya kazi kwenye mchezo huo wa ligi.
Mashabiki waliowengi wa PSG wanadai kuwa mshambuliaji amechoka kutokana na kutumika katika michezo iliyopita kitu ambacho Ancelot anadai kuwa na imani ya nyota huyo alikuwa fiti kwa asilimia 80 za kucheza vizuri.
Tangu ajiunge na PSG Zlatan mwenye umri wa miaka 31 anaongoza kwa magoli kwa kufunga magoli 9 katika michezo nane ya ligi nchini ufaransa sambamba na goli moja la ligi ya mabingwa barani ulaya alilofunga katika mchezo dhidi ya  Dyanamo Kiev.

0 comments:

Post a Comment