NJOMBE KUCHEZA NA MBEYA CITY BADALA YA MAJIMAJI.



Kikosi cha timu Njombe mji, hapo kesho kitashuka dimbani kucheza na timu ya Mbeya City kwenye uwanja wa Amani uliopo mjini Makambako.
Akizungumza na Mwananchi katibu mkuu wa timu ya Njombe Mji, Obeid Mwakasungura,amesema mchezo huo walipanga kucheza na timu ya Majimaji ya Songea lakini imeshindikana kutokana na kikosi cha Wanarizombe kushindwa kupatwa na udhuru ulioikwamisha timu hiyo kufika mkoani Njombe.
Mwakasungura amesema kuwa viongozi wa Mbeya City wamethibitisha kufika na kucheza mchezo huo wa kirafiki kwaajili ya maandalizi ya ligi ya mkoa kwa timu ya Njombe mji na ligi daraja la kwanza kwa timu ya Mbeya City toka jijini Mbeya.
Katika mchezo uliozikutanishia timu hizo mbili kwenye uwanja wa Amani, timu ya Njombe mji ilifungwa magoli matatu kwa moja na Mbeya City.

0 comments:

Post a Comment