WALCOT KUFANYIWA VIPIMO ZAIDI



 Theo Walcott
walcot akiwa chini baada ya kuumia kwenye mchezo wa jana.
Kocha wa timu ya taifa ya England, Roy Hogson, amesema mshambuliaji wake wa Pembeni Theo Walcot, atafanyiwa uchunguzi zaidi kabla ya kuukabili mchezo wa jumanne.
Hogson amesema hayo wakati akizungumzia jeraha la kifua alilolipata mchezaji huyo kwenye mchezo wa jana dhidi ya San Marino, ambao Walcot aliumia baada ya kugongana na kipa wa Marino, Aldo Simoncini.
Akizungumzia maendeleo mchezo huo,Hogson amesema usiku wa jana alilazwa hospali na hii leo anataraji kupigwa picha ya X-ray kwaajili ya uchunguzi zaidi wa afya yake.
Ushindi wa magoli 5 alioupata jana, Hogson amesema ni ushindi faraja kwao na wanajipanga kusaka ushindi zaidi katika michezo inayofuta ukiwemo wa jumann dhidi ya Poland.
Taarifa Soccerway

0 comments:

Post a Comment