Ligi kuu ya Tanzania bara kuendelea
hapo kesho kwa michezo kadhaa kuchezwa nchini kwenye viwanja tofauti.
Katika uwanja wa taifa jijini Dar es
Salaam klabu ya Azam itacheza na vinara wa ligi hiyo Simba, wakati kule mjini
Arusha timu ya Yanga itakuwa na kibarua kigumu mbele ya maafande wa JKT Oljoro.
Michezo mingine ya ligi hiyo ni African
Lyon kucheza na Kagera Sugara kwenye uwanja wa Azama Complex uliopo mbagala.
Ilhali kwenye uwanja wa Mabatini timu ya Ruvu Shooting itakuwa mwenyeji wa
Polisi Morogoro.
Mchezo kati ya Mgambo JKT na Tanzania
Prisons umeiahirishwa baada kufuatia timu ya Prisons kupata Ajali iliyotokea
usiku wa juzi eneo la Hale jijini Tanga.
0 comments:
Post a Comment