
Steward wakati wa uhai wake.
Mwalimu
mkongwe wa mchezo wa ngumi, Emanuel Steward wa marekani,amefariki dunia mchana
wa jana akiwa hospitalini jijini Chicago nchini humo.
Akitoa
taarifa ya kifo hicho, raisi wa shirikisho la ngumi za nchiniMarekani HBO, Ken
Herishman amesema kifo hicho kimetokea wiki kadhaa baada ya kocha huyo kulazwa
hospitali kwaajili ya kufanyiwa upasuaji wa ugonjwa wa kansa.
Steward
amefariki akiwa na umri wa mia 68 huku akiwa na rekodi ya kuwafundisha mabondia
mbalimbali ulimwenguni wakiwemo Wilfred Benitez, Julio Cesar Chavez, Oscar de
la Hoya, Evander Holyfield, Mike McCallum and James Toney.
Mpaka
anakutwa na mauti Steward alikuwa ndiye kocha mkuu wa bondia wa Ukraine Vladmil
Klitschko ambaye kwa sasa anatikisa ulimwengu kwa ubora wa mchezo huo.
Katika
kupokea msiba huo mzito Klitscho amesema kifo cha Steward ni pigo kwake huku
akikiri kuishi naye kwa mafanikio na marehemu alikua akiipenda kazi ya Vladmir
kutokana na jinsi anavyojituma katika mechi zake.
Katika
kipindi chake cha ubondia Steward mwaka 1980 alikuwa bingwa dunia baada ya
kumpokonya ubingwa huo Hilmer Henky aliekuwa akitamba kipindi hicho na hadi
anafariki Stewarda ameacha kitengo cha mazoezi ya ngumi kinacho julikana kwa
jina la Kronky Gym iliyopo jijini Detrot nchini Marekani.
0 comments:
Post a Comment