
St Gerge`s Park
Chama cha soka cha nchini England FA, kimefungua kituo cha
kukuza na maendeleo ya soka nchini humo kinachojulikana ka St George`s Park
Complex.
Mwenyekiti wa FA David Bernestein amesema kituo hicho chenye
upana wa ekali 330, na kimegharimu kiasi cha paundi milioni 105 katika
kukamilisha ujezi wake kule jijini Stafford shire.
Amesema lengo ni kuwa na wachezaji wengi wa kimataifa na
wenye viwango bora ndio maana wameweka mafunzo ya ukocha, madawa pamoja
saikolijia ya michezo katika kituo hicho.
Timu ya taifa ya England inayojiandaa kucheza na San Marino
katika mchakato wa kutafuta tiketi ya kombe la dunia wiki hii itakuwa ya kwanza
kufanya maandalizi kwenye kituo hicho kipya cha soka
0 comments:
Post a Comment