
Moja ya harakati za mechi za ligi kuu bara inavyokuwa.
Michuano ya Ligi Kuu
ya Vodacom inaendelea kesho (Oktoba 13 mwaka huu) kwa timu kumi kupambana
kwenye viwanja vitano tofauti katika raundi ya saba ya ligi hiyo yenye timu 14.
Polisi Morogoro
itaikaribisha Azam kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati mwamuzi wa
FIFA, Oden Mbaga atakuwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya
kuchezesha mechi kati ya wenyeji Tanzania Prisons na Oljoro JKT.
Jijini Tanga, Simba
itakuwa mgeni wa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani katika mechi
itakayochezeshwa na mwamuzi Simon Mberwa kutoka Pwani akisaidiwa na Godfrey
Kihwili na Abdallah Uhako wote kutoka Arusha.
Mechi nyingine za
kesho ni Ruvu Shooting dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa Mabatini mjini
Mlandizi, na Mtibwa Sugar watacheza na Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa
Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Wakati huo huo, Azam
imeomba mechi zake za nyumbani dhidi ya Yanga na Simba zichezwe kwenye uwanja
wake wa Azam Complex ulioko Chamazi badala ya Uwanja wa Taifa.
Nayo Ruvu Shooting
imeomba mechi yake ya ugenini dhidi ya Yanga ya Oktoba 20 mwaka huu ichezwe
Uwanja wa Taifa badala ya Uwanja wa Azam Complex.
Maombi hayo
yatawasilishwa kwenye kikao cha Kamati ya Ligi ya TFF kinachotarajiwa kufanyika
kesho (Oktoba 13 mwaka huu) kwa ajili ya kufanyiwa uamuzi.
0 comments:
Post a Comment