
Mwenyekiti waa FA,David Bernstein
Mlinzi wa klabu ya
Chelsea na Ashley Cole, amefutiwa adhabu ya kufungiwa kuchezea timu ya
taifa baada ya kuomba radhi kutokana na kauli aliyo itoa hivi karibuni katika
mtandao wa kijamii.
Mwenyekiti wa chama
cha soka nchini England FA, David Bernstein amesema, usiku wa jana Cole ameomba
radhi juu ya kosa la utovu wa nidhamu alilolifanya.
Amesema kutoka na maamuzi hayo aliyoyafanya Cole yupo huru
kulitumikia taifa lake huku kukiwa na uwezekano wa kuwemo kwenye kikosi cha
kwanza kitakacho anza dhidi ya San Marino siku ya Ijumaa.
Juma lililopita Cole aliandika maneno ya kejeli kwenye mtandao
wa kijamii unaojulikana kama Twitter, kwamba FA wamefanya vizuri na ushahidi
wake ulikuwa wa uongo juu ya tuhuma za ubaguzi wa rangi zinazo mkabili, Jonh
Terry.
0 comments:
Post a Comment