Wagombea 13 kati ya
15 waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye Chama cha Mpira wa
Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) wamepitishwa baada ya usaili uliofanyika juzi
katika ofisi za TFF.
Kwa mujibu wa
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala, amesema waliopitishwa
kwenye nafasi ya uenyekiti ni Isabellah Kapera, Joan Minja na Lina Kessy.
Makamu Mwenyekiti ni
Rose Kisiwa wakati wanaowania nafasi ya Katibu Mkuu ni Amina Karuma na Cecilia
Makafu. Mgombea pekee wa nafasi ya Katibu Msaidizi, Macky Mhango wakati nafasi
ya Mhazini ampepita Rose Msamila.
Furaha Francis na
Zena Chande watawania nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa (TFF) wakati
waliopita nafasi za ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TWFA ni Triphonia Ludovick
Temba, Rahim Maguza na Sophia Charles.
Mchakato wa uchaguzi
wa TWFA uko katika kusikiliza rufani zitakazo anzia Oktoba 15-17 mwaka huu.
Rufani zinatakiwa zifike kwa Katibu Mkuu wa TFF kabla ya saa 10 kamili jioni ya
Oktoba 17 mwaka huu.
Uchaguzi unatarajiwa
kufanyika Novemba 4 mwaka huu ni Julliet Mndeme na Jasmin Soud walioomba ujumbe
wa Mkutano Mkuu wa TFF. Wagombea hao ambao pia walikuwa wamewekewa pingamizi
hawakufika kwenye usaili.
Chanzo TFF makao makuu.
0 comments:
Post a Comment