Yanga na Kagera wakimenya msimu uliopita.
Wakati hii leo
tukishudia michezo miwili ya ligi ya ligi kuu ya Tanzania bara ambayo ni
African Lyon dhidi ya Azam fc huku Ruvu Shooting ikicheza na Coast unioni
hapo jana Kamati ya
Ligi imetangaza kusogeza mbele kwa siku moja mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati
ya Kagera Sugar na Yanga iliyokuwa ichezwe kesho (Oktoba 7 mwaka huu) mjini
Bukoba kutokana na Uwanja wa Kaitaba kuwa na shughuli nyingine za kijamii.
Sasa mechi hiyo
itachezwa Jumatatu (Oktoba 8 mwaka huu) kwenye uwanja huo huo. Mabadiliko hayo
pia yameathiri mechi kati ya Toto Africans na Yanga iliyokuwa ichezwe Oktoba 10
mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Mechi hiyo sasa itachezwa Oktoba
11 mwaka huu.
Wakati huo huo, Kamati
ya Ligi imewaondoa waamuzi watatu wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa kushindwa
kumudu michezo waliyopangiwa. Waamuzi hao ni Mathew Akrama wa Mwanza
aliyechezesha mechi namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na
Simba iliyochezwa Oktoba 3 mwaka huu.
Wengine ni Paul
Soleji wa Mwanza aliyechezesha mechi kati ya Simba na Tanzania Prisons, na
mwamuzi msaidizi namba mbili kwenye mechi hiyo Mwarabu Mumbi wa Morogoro. Pia
mwamuzi msaidizi namba mbili wa mechi ya Yanga na Simba, Ephrony Ndissa wa Dar
es Salaam amepewa onyo.
Kamishna wa mechi
namba 28 kati ya Yanga na African Lyon, Pius Mashera ameondolewa kwenye orodha
ya makamishna wa ligi hiyo kwa kuchelewa kufika kwenye kikao cha maandalizi ya
mechi (Pre match meeting) na uwanjani.
Vilevile Mashera
kwenye ripoti yake aliwasilisha malalamiko dhidi ya msimamizi wa kituo cha Dar
es Salaam, na kwa vile suala hilo ni la kinidhamu ametakiwa alipeleke kwenye
Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF.
Nayo Simba imepigwa
faini ya jumla ya sh. 600,000 kwa kuchelewa kufika kwenye pre match meeting ya
mchezo wao dhidi Tanzania Prisons (sh. 100,000) na kwa washabiki wake kuwatupia
chupa za maji waamuzi wa mechi hiyo (500,000).
Pia Kamati ya Ligi
imeagiza kuwa kwa vile suala la kipa Shabani Kado wa Mtibwa Sugar kudaiwa
kumpiga kiongozi mmoja wa Ruvu Shooting mara baada ya mechi kati ya timu hizo
iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex ni la kinidhamu lipelekwe kwenye Kamati ya
Nidhamu na Usuluhishi ya TFF.
0 comments:
Post a Comment