Vick Macha enzi za uhai wake akiwa katika hifadhi Taifa Ruaha wakati
wa ziara ya wanahabari Iringa kuhamasisha utalii wa ndani kwa watanzania
Marehemu
Vicky Macha kulia akiwa katika mkutano wake wa mwisho wa umoja wa vilabu
vya waandishi wa habari nchini Tanzania (UTPC) ambapo pia alikabidhiwa
michango ya rambi rambi ya kifo cha Daudi Mwangosi .
Marehemu
Vicky Macha ambaye amefariki asubuhi ya leo katika Hospitali ya mkoa wa
Iringa alizaliwa tarehe 14 /2/1972 mwili wake utaagwa kesho
katika katika Hospitali ya mkoa wa Iringa na msiba kwa sasa
upo eneo ya Kibwabwa Shapria kata ya Kitwiru katika Manispaa ya
Iringa ambako alikuwa akiishi
Zoezi
la kuaga mwili litaanza saa 6 mchana kabla ya kuondoka majira ya saa 8
mchana kuelekea Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kwa Mazishi .
Zoezi
la kuaga mwili wa marehemu litaanza majira ya saa 6 mchana
ili kuwawezesha wale waliopo katika msafara kuanza safari mapema
kwa mujibu wa marehemu Vicky Bw Philimon Shirima ambaye amezungumza na mtandao
huu wa www.francisgodwin.blogspot.com jioni hii
kuwa .
Mwanahabari
Vicky Macha ameacha watoto wawili huku mtoto mmoja wa
kike akiwa na miaka 16 na wa kiume akiwa na miaka 7.
Tasnia
ya habari mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla imepata pigo
kubwa kwa kuondokewa na mwanahabari Vicky Macha ambaye alikuwa akiandikia
gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa na pia alikuwa ni mweka hazina wa klabu
ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) .
Vicky
Macha atakumbukwa kwa jitihada zake mbali mbali alizozifanya katika kudumisha
IPC na tasnia ya habari kwa ujumla hata kupendwa na kila mdau wa habari kwa
kazi zake .
Mtandao
huu wa www.francisgodwin.blogspot.com pamoja na
kuwa msiba huu ni mkubwa zaidi kutokana na Vicky Macha kuwa ni kiongozi
mwenzangu ila bado naweza kusema kila nasi itaonja mauti Vicky Ametangulia
kuandaa makao ni zamu ya nani ni mwenyezi Mungu anajua hivyo tukeshe
tukiomba maana hatujui siku wala saa ya kuianza sasfari kwenda
kuanza makao mapya.
JINA
LAKE BWANA NA LIHIMIDIWE DAIMA
TAARIFA HII IMETOKA KWENYE MTANDAO WA FRANCIS GODWIN.
0 comments:
Post a Comment