Vita ya Msigwa na Mwakalebela imehamia kwenye soka.



                
         Mch. Msigwa akiwa katika moja harakati za michezo
Uongozi wa chama cha soka wilaya ya Iringa mjini umemtangaza aliekuwa katibu mkuu wa TFF Fredirick Mwakalebela, kuwa mdhamini mkuu wa ligi ya wilaya hiyo inayotaraji kuanza mapema mwezi huu.
 
Akizungumza na Blog hii, katibu mkuu wa chama soka wilayani humo IMDFA, Bakari Kamtande amesema udhamini wa Mwakalebelela umepitishwa kufuatia makubaliano ya vipengele vilivyopo kwenye mkataba wao wa ligi hiyo.
Amesema Mwakalebela alikubaliana na vipengele vyote vya mkataba huo sambamba na kutaka kudhamini ligi hiyo kwa miaka mitatu kitu ambacho FA wilaya ilikataa na kumpatia miaka miwili pekee ya kudhamini ligi hiyo.
                      

                                     Mwakalebela
Kwa upande mwingine Kamtande amesema kuwa amesikitishwa na kauli za mbunge wa jimbo la Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa juu ya kukilalamikia chama cha soka juu ya kuitengua dhamira yake kudhamini ligi hiyo, amesema Mch. Msigwa alitamka maneno ya kukidharirisha chama cha soka katika mkutano wa hadhara kuwa  IMDFA imeingiza siasa na mianya ya rushwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu wilaya Iringa.
Akitoa ufafanuzi wa mkataba wake kati ya IMDFA na Msigwa, Kamtande amesema kuwa walitoa nafasi kwa mbunge huyo kudhamini ligi ila alikataa kukubali baadhi ya vipengele vya mkataba kiasi ambacho kilipelekea maamuzi ya chama kumkabidhi nafasi hiyo Mwakalebela aliekubali vipengele vyote sanjari na kudai mkataba wa miaka mitatu ila chama kilibariki kumpa mkataba wa miaka miwili pekee kwa mitatu ni mingi zaidi.
Aliongeza Kamtande kuwa anaheshimu mchango wa mbunge huyo katika soka la Iringa ila anaiondoa heshima yake kutokana na uwajibikaji mbovu wa waratibu wa mbunge huyo akiwemo Abu Changawa ambaye hivi karibuni TFF iliitaka IRFA kumchukulia hatua kwa kosa la kufanya vurugu kwenye uchaguzi wa chama cha soka mkoa .
Mwishoni mwa jumalililopita Mch. Msigwa aliwatangazia wananchi kwenye mkutano wa hadhara kuwa mianya ya rushwa na siasa iliyoingizwa kwenye soka imemnyima nafasi ya kukuza soka la Iringa huku akionesha hadharani vifaa vichezo ikiwemo Jezi na mipira ambavyo alipanga kutoa kwa vilabu kama sehemu ya udhamini wa ligi hiyo.
Nilivyozungumza naye kwa njia ya simu, Fredirick Mwakalebela, alikubali kuwa ameombwa kudhamini ligi ila bado hajatoa maamuzi juu kusaini mkataba na hajajua kama kuna mvutano kati ya chama na Mch Msigwa.
MWISHO.

0 comments:

Post a Comment