Bondia
Thomas mashali wa Tanzania na Mganda Medi Sebyala wanatarajiwa kupima uzito
Jumamosi saa nne asubuhi katika ukumbi wa Friends Corner manzese tayari kwa
mpambano wao utakaofanyika oktoba 14 Jijini Dar es salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mratibu wa mpambano huo unaosimamiwa na oganaizesheni ya
Ngumi za kulipwa nchini TPBO Regina Gwae amesema upimaji huo ndo hatua ya
mwisho kuelekea kujua nani atanyakua ubingwa wa Afrika Mashariki na kati.
Amesema
mbali na mabondia hao pia mabondia wa mapambano ya utangulizi ambapo Abdul
Awilo atapambana na Shedrack Juma, selemani shaaban atapambana na Hamisi Mohamed
Jonas Segu atapambana na Ibrahim Class wkati Charles mashali atapambana na
Teacher Aron nao watapima.
Amesema
maandalizo yote yamekamilika ikiwemo waamuzi wenye sifa za kuchezesha mapambano
ya kimataifa wameshapatikana na majina yao yatatangazwa jumamosi.
Mgeni
rasmi katika pambano hilo ni Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi wa Kinondoni
Charles Kenyela ambaye anatarajiwa kuambatana na wageni wengine maalum wakiwemo
wabunge.
Amesema
anashukuru kwa ushirikiano wa viongozi katika maandalizi na hatimaye maandalizi
yanaelekea ukingoni na pambanolinatarajiwa kuvuta hisia za watu wengi na
wapenzi wa ngumi jijini Dar es Salaam.
Regina
alishukuru kampuni ya Promasidor wasambazaji wa SOSSI Poa, Gazeti la Jambo
leo,City Sports Lounge na Times Fm kwa kuwa bega kwa bega kuhakikisha pamnano
hili linafanikiwa na kusema milango bado iko wazi kwa wadau kujitokeza
kufanikisha mchezo huo ambao ni chanzo cha ajira kwa vijana.
Taarifa na Zainab Kiluwale.
0 comments:
Post a Comment