Kamati ya Uchaguzi ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekamilisha usikilizaji rufani
zilizokatwa dhidi ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA.
Ili kujiridhisha
kuhusu uamuzi wote uliofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya DRFA kuhusu waombaji
uongozi wote wa DRFA waliopitishwa na ambao hawakupitishwa na Kamati ya
Uchaguzi ya DRFA, Kamati itatangaza uamuzi wake kuhusu mchakato mzima wa
uchaguzi wa DRFA siku ya Jumanne, Oktoba 16, 2012.
Kutokana na hali
hiyo, Uchaguzi wa DRFA uliokuwa ufanyike Oktoba 14, 2012 umeahirishwa hadi hapo
uamuzi kuhusu uchaguzi huo utakapotangazwa Jumanne, Oktoba 16, 2012.
Angetile Osiah
Katibu Mkuu
Katibu- Kamati ya Uchaguzi TFF
0 comments:
Post a Comment