Ligi daraja la kwanza
Tanzania bara itaanza kuchezwa rasmi Oktoba 20 mwaka huu kwa mgawanyo wa
makundi matatu yenye timu nane nane kwa kila kundi moja
Akizungumzia hilo
msemaji wa TFF Boniface Wambura amesema uamuzi huo umetokana na kikao cha kamati
ya ligi kilichoketi jana jiji Dar es Salaam na kupanga tarehe hio sambamba na
kuvitaka vilabu kulipa ada ya ushiriki ambayo ni shilingi laki mbili kabla ya
Oktoba 13 mwaka huu.
Amesema ligi hiyo
itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini kwa timu zote 24, na bingwa wa kila
kundi atapata nafasi ya kupanda ligi kuu msimu ujao
Katika ligi hiyo
kundi A lina timu za Burkina Moro, Kurugenzi, Majimaji, Mbeya City, Mlale JKT,
Mkamba Rangers, Polisi Iringa na Small Kids ya Rukwa, wakati kundi B linaundwa
na Ndanda FC, Ashanti United, Green Warriors, Moro United, Polisi, Tessema,
Transit Camp na Villa Squad zote za Dar es Salaam
Kwa upande wa kundi C
ni Kanembwa JKT ya Kigoma, Morani ya Manyara, Mwadui ya Shinyanga, Pamba ya
Mwanza Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Tabora na Rhino Rangers ya Tabora.
0 comments:
Post a Comment