JESHI LA SERBIA LA KINUKISHA KWA WACHEZAJI WA ENGLAND



Jeshi la polisi la nchini Serbia limewatia hatiani watu 12 wakiwemo wachezaji wawili wa timu ya taifa ya England chini ya umri wa miaka 21 kwa tuhuma kusababisha vurugu kwenye mchezo kati ya England na Serbia wakufuzu fainali za ulaya mwaka 2013.
Jeshi hilo halikuweka bayana majina ya watu hao ila imeeleza kuwa katika orodha hiyo wamo wachezaji watano wa timu ya Serbia, makocha wa wasaidizi wa timu zote mbili sambamba na wachezaji wawili wa England.
Kwa upande mwingine jeshi limesisistiza kuwa walioingizwa katika kesi hiyo ya jinai ndio walio thibitishwa na kuanzisha vurugu kutokana na uchunguzi uliofanywa na polisi wa jiji la Krusevac kwa muda wa wiki mbili
Kwa upande wa chama cha soka cha nchini England FA, kimesema kuwa mpaka sasa hawajapokea maelezo yoyote juu ya kesi hiyo na kwasasa wanasubiri maelezo kamili ili waweze kutoa tamko.
Katika mchezo huo wa kuwania tiketi ya michuano ya ulaya ya mwaka 2013 uliochezwa jijini Krusevac nchini Serbia, Octoba 16 mwaka England iliifunga Serbia magoli 1kwa 0

NJOMBE MJI KUCHEZA NA BURKINA FASO



Timu ya Njombe mji toka mkoa mpya wa Njombe hapo kesho itashuka dimbani kucheza na timu ya Burkinfaso ya Morogoro katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa kwenye uwanja wa Amani.
Akizungumza na Ebony FM katibu wa Njombe Mji, Kaini Nyigu amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika huku akiwataka wadau kujitokeza kwenye mchezo huo.
Huu ni mchezo wa nne wa mkubwa wa kirafiki kwa timu ya Njombe mji ambayo imajipanga vilivyo kuhakikisha inafanya vema kwenye michuano ya ligi ya wilaya.

HII NDIO ILIYOSHUSHWA LEO NA TASWA.



Chama cha waandishi wa habariza michezo nchini Taswa kimepokea nafasi ya mafunzo kwa waandishi wa habari wanawake yaliyoandaliwa na kamati ya Olimpiki ya kimataifa IOC, na muunganio wa kamati za Olimpik za Afrika ANOCA kupitia kamati ya Olimpic Tanzania TOC.
Akizungumzia hilo katibu wa Taswa Amir Muhando amesema mafunzo hayo yataanza kufanyika rasmi Desemba 10 na 11 mwaka huu katika jiji la Nairobi nchini Kenya.

Amiri amesema TASWA imepewa nafasi za waandishi wa habari wanawake watatu washiriki kwenye mafunzo hayo na imepokea barua hiyo leo wakati siku ya Ijumaa ya wiki hii majina yawe yameshatumwa kwa wahusika.

baada ya kutolewa nafasi hizo chache  Taswa imewataka waandishi wanawake wenye nia na muda wa kushiriki wawasilishe CV zao kabla ya Ijumaa (Novemba 2, 2012) saa sita mchana ofisini kwa Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto (Hifadhi House ghorofa ya 9 zilipo ofisi za JamboLeo, Posta)  au kwangu mimi ofisi za Daily News Tazara, Dar es Salaam.

Masharti ya mafunzo ni kuwa yataendeshwa kwa lugha ya Kingereza na Kifaransa, lakini pia watakaoshiriki wawe tayari kuja kutoa elimu watakayaoipata huko kwa wenzao pindi watakaporudi nchini.

Suala la CV ni la umuhimu kupita maelezo, kwani baada ya hapo mchana siku hiyo TASWA itateua majina matatu na kuyatuma TOC kwa taratibu nyingine.

MWALIMU WA KLITSCHKO AFARIKI DUNIA.



 Emanuel Steward
                        Steward wakati wa uhai wake.
Mwalimu mkongwe wa mchezo wa ngumi, Emanuel Steward wa marekani,amefariki dunia mchana wa jana akiwa hospitalini jijini Chicago nchini humo.
Akitoa taarifa ya kifo hicho, raisi wa shirikisho la ngumi za nchiniMarekani HBO, Ken Herishman amesema kifo hicho kimetokea wiki kadhaa baada ya kocha huyo kulazwa hospitali kwaajili ya kufanyiwa upasuaji wa ugonjwa wa kansa.
Steward amefariki akiwa na umri wa mia 68 huku akiwa na rekodi ya kuwafundisha mabondia mbalimbali ulimwenguni wakiwemo Wilfred Benitez, Julio Cesar Chavez, Oscar de la Hoya, Evander Holyfield, Mike McCallum and James Toney.
Mpaka anakutwa na mauti Steward alikuwa ndiye kocha mkuu wa bondia wa Ukraine Vladmil Klitschko ambaye kwa sasa anatikisa ulimwengu kwa ubora wa mchezo huo.
Katika kupokea msiba huo mzito Klitscho amesema kifo cha Steward ni pigo kwake huku akikiri kuishi naye kwa mafanikio na marehemu alikua akiipenda kazi ya Vladmir kutokana na jinsi anavyojituma katika mechi zake.
Katika kipindi chake cha ubondia Steward mwaka 1980 alikuwa bingwa dunia baada ya kumpokonya ubingwa huo Hilmer Henky aliekuwa akitamba kipindi hicho na hadi anafariki Stewarda ameacha kitengo cha mazoezi ya ngumi kinacho julikana kwa jina la Kronky Gym iliyopo jijini Detrot nchini Marekani.

MICHEZO YA LIGI KUU BARA HAPO KESHO.



Ligi kuu ya Tanzania bara kuendelea hapo kesho kwa michezo kadhaa kuchezwa nchini kwenye viwanja tofauti.

Katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam klabu ya Azam itacheza na vinara wa ligi hiyo Simba, wakati kule mjini Arusha timu ya Yanga itakuwa na kibarua kigumu mbele ya maafande wa JKT Oljoro.

Michezo mingine ya ligi hiyo ni African Lyon kucheza na Kagera Sugara kwenye uwanja wa Azama Complex uliopo mbagala. Ilhali kwenye uwanja wa Mabatini timu ya Ruvu Shooting itakuwa mwenyeji wa Polisi Morogoro.

Mchezo kati ya Mgambo JKT na Tanzania Prisons umeiahirishwa baada kufuatia timu ya Prisons kupata Ajali iliyotokea usiku wa juzi eneo la Hale jijini Tanga.