Uongozi wa timu ya Lipuli ya mkoani Iringa mwisho umetangaza
kamati itakayosimamia masuala ya usajili na ufundi katika klabu hiyo kongwe ya
mkoani Iringa,
Akizungumza na mwananchi mwenyekiti wa klabu hiyo iliyobeba
jina lenye maana ya Ngome ya Mkwawa Abnery Mrema amemtaja ndugu Pascal Bella
kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo huku Ahmadi Lulanga akiwa makamu mwenyekiti
wakati katibu mkuu akiteuliwa aliekuwa katibu wa Polisi Iringa msimu uliopita
Willy Chikweo.
Kwa upande wa wajumbe wa kamati hiyo ni Edna Kajiba ambaye
pia ni katibu wa Netball mkoani iringa, Mheshimiwa Mbata, Mengi Kifyoga pamoja
na Benson Massiagi.
Katika taarifa yake hiyo Mrema aliongeza kwa kumtaja Ahmadi
Lulanga kuwa kocha wa Lipuli, Pascal Bela kuwa mkurugenzi wa Ufundi na Agustino
Msigwa kuwa msemaji wa timu wa timu hiyo.
Mrema amemaliza kwa kusema kuwa uteuzi huo umezingatia
maamuzi ya kikao kilichofanyika Desemba 30 kujadili maendeleo ya klabu ya
Lipuli huku wakiwa na mikakati mizito ya kuhakikisha hadi kufikia mwishoni
mwaka 2013 wawe na uhakika wa kurejea kwenye ligi kuu ya Tanzania bara kuwa
mwaka 2015.
Kwa sasa Lipuli ya Iringa inakabiliwa na kibarua kigumu cha
kusaka ubingwa wa ligi ya mkoani wa Iringa walioupoteza kwa rufaa ya njombe mji
mwaka 2010.
0 comments:
Post a Comment