FLETCHER ARUDI TENA KWENYE MATIBABU.



       
Manchester United midfielder Darren Fletcher
Klabu ya Manchester united imethibitisha kumkosa kiungo wake Darren Fletcher katika michezo yake iliyosalia kufuatia kurejea katika matibabu ya vidonda vya tumbo..
Manchester united imeripoti kuwa Fretcher mwenyer umri wa miaka 28, atakosa michezo hiyo kufuatia kuendelea na upasuji uaoendelea ili kutatua tatizo alilonalo la vidonda wa vya tumbo.
Ukizungumzia tukio hilo uongozi wa Manchester united umethibitisha kuwa upasuaji wa Fletcher ulikuwa katika mpango ili kukamilisha matibabu ya mchezaji huyo ambaye ni tegemeo kubwa katika safu ya kiungo.
Aidha kocha wa timu ya Scotland  Gordon Strachan amewataka washabiki kuwa wavumilivu huku akisisitiza kuwa kutibiwa kwa Fretcher ni mafanikio kwa taifa na klabu yake ya Manchester united.
Mwishoni mwaka 2011 nahodha huyo wa Scotland,alipumzika kwa mara ya kwanza kabla ya kurejea msimu huu na kucheza michezo 13 ya ligi kuu ya England.

0 comments:

Post a Comment