WENGER KUFANIKISHA DILI NA WALCOTT



 
Meneja wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger, amesisitiza kukamilisha usajili wa nyongeza kwa mshambuliaji wake Theo Walcott kabla ya kufungwa dirisha dogo la usajili linalo endelea kufanya kazi hadi mwishoni mwa mwezi huu.
Wenger amesema kwa uzoefu wake wa kufanya mazungumzo anasilimia 99 mpaka sasa za kumalizaa vizuri na mshambuliaji huyo huku akisisitiza kuwa huenda mwishoni mwaka wiki hii usajili wake utaambatana na mchezo wa ligi dhidi ya Chelsea.
Moja kati ya vigezo vya Walcot mwenye umri wa miaka 23 kutaka kuongeza mkataba ni kupewa nafasi kama mshambuliaji wa mwisho na kulipwa kiasi cha mshahara wa paundi  kali moja kwa wiki.
Lakini Wenger aliyevuma kutaka kuwasajili Wilfred Zaha wa Crystal Palace na Edinson Cavani wa Napoli ili kuziba pengo la mchezaji huyo wa kiingereza hakusita kuelezea dhamira ya kumuacha mchezaji huyo aondoke kama mchezaji huru endapo hatokubali mkataba mpya.

0 comments:

Post a Comment