
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom
inaingia raundi ya 15 kesho (Januari 30 mwaka huu) kwa mechi mbili ambapo Azam
iliyo katika nafasi ya pili nyuma ya Yanga itakuwa mwenyeji wa Toto Africans ya
Mwanza.
Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa
Chamazi, Dar es Salaam huku Azam ikisaka ushindi ili kuikaribia Yanga
inayoongoza wakati Toto Africans inayonolewa na John Tegete ikitaka kurekebisha
makosa ya kupoteza mechi yake iliyopita dhidi ya Oljoro JKT.
Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri
Abeid jijini Arusha utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Oljoro JKT dhidi ya
wageni Kagera Sugar kutoka Bukoba mkoani Kagera itakayochezeshwa na mwamuzi
Jacob Adongo wa Musoma.
Ushindi kwa Oljoro JKT yenye
pointi 17 utaihakikishia kubaki katika nafasi yake ya nane wakati Kagera Sugar
inayofundishwa na kocha mkongwe Abdallah Kibaden utaifanya ipige hatua moja
mbele katika msimamo wa ligi.
Ligi itaendelea tena Jumamosi
(Februari 2 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo vinara Yanga wataumana na Mtibwa
Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Polisi Morogoro
ikiikaribisha African Lyon mjini Morogoro.
Nazo Mgambo Shooting ya Tanga na
Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
0 comments:
Post a Comment