MRFA KUSIMAMIA UCHAGUZI WA TAFCA MORO.



Chama cha makocha mkoa wa Morogoro(TAFCA) kinatarajia  kutumia kamati ya uchaguzi ya chama cha soka mkoa wa  Morogoro (MRFA) kusimamia uchaguzi wake baada ya kukamilisha rasimu ya katiba inayolingana na ile ya chama hicho taifa.
Katibu wa TAFCA Morogoro Edward Hizza  alisema kuwa chama hicho kimeshakamilisha rasimu hiyo ya katiba lakini kutokana na kukosa kamati ya kusimamia uchaguzi wake. wamelazimika kuitumia kamati ya uchaguzi ya MRFA ili kuweza kusimamia uchaguzi huo.

Hata hivyo alisema kuhusu viongozi waliopo madarakani kama watagombea au vinginevyo, hawawezi kulizungumzia kwa sasa, ingawa akakiri muda wao wa miaka minne wa kukaa madarakani kuwa ulishamalizika huku baadhi ya waliokuwa viongozi wakiwa wamepoteza maisha.
Nafasi zitakazo waniwa kwenye uchaguzi huo ambao mpaka sasa haujapangiwa Tarehe, ni mwenyekiti, Makamu mwenyekiti,katibu mkuu, katibu msaidizi , mweka hazina  na msaidizi wake pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa.

0 comments:

Post a Comment