Ochieng kushoto na Akuffo kulia wakitambulishwa baada ya kusajiliwa.
Kamati ya Sheria, Maadili na
Hadhi za Wachezaji iliyokutana Januari 19 mwaka huu chini ya Mwenyekiti wake
Alex Mgongolwa imeliondoa shauri lililokuwa mbele yake dhidi ya klabu ya Simba
lililowasilishwa na wachezaji Pascal Ochieng na Daniel Akuffo baada ya pande
hizo kufikia makubaliano.
Wachezaji hao kutoka Kenya na
Uganda waliwasilisha malalamiko mbele ya kamati wakipinga kukatizwa mikataba
yao bila kulipwa stahili zao. Hata hivyo, pande zimefikia makubaliano ya
kuvunja mikataba nje ya kamati, na wachezaji hao kulipwa stahili zao.
Pia Simba imekiri kudaiwa na
wachezaji Shija Mkina, Swalehe Kabali, Victor Costa na Rajab Isiaka na kuahidi
kuwalipa wachezaji hao wakati Coastal Union na mchezaji wake Mohamed Issa
wamefikia makubaliano ya malipo, hivyo kuvunja mkataba kati ya pande hizo
mbili.
0 comments:
Post a Comment