Timu ya Azam FC kesho
Jumanne itamalizia ziara yake ya mechi za kirafiki jijini Nairobi kwa kucheza
dhidi ya K.C.B kwenye Uwanja wa City.
Kikosi cha Azam FC
kipo jijini Nairobi kwa ziara ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya
soka Tanzania bara pamoja na michuano ya kombe la Shirikisho Afrika, tayari
kimeshacheza miwiwli ya kitaifa ya kirafiki dhidi ya AFC Leopards na kufungwa
mabao 2 -1 mawili kisha wakachomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya
Sofapaka FC.
Kikosi cha Azam FC
kinatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam siku ya jumatano, baada ya mchezo wa
kesho dhidi ya KCB na kusubiri michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara raundi ya
pili.
Naye Kocha Stewart Jahn
Hall amesema wachezaji wote wako safi kwa mchezo huo dhidi ya KCB utakao chezwa kesho kwenye uwanja wa City wenye
nyasi bandia sawa na uwanja wao wa chamazi.
Wakati Azam
wakitarajiwa kurejea nyumbani siku ya jumatano kwa ajili ya kusubiri mzunguuko
wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, kamati ya ligi ya shirikisho al soka
nchini TFF inasubiriwa kutoa kauli ya kuendelea kwa ligi hiyo kama
ilivyopangwa, ama kusogeza mbele tarehe.
Afisa habari wa TFF Bonifas Wambura amesema kamati ya ligi
inasubiriwa kufanya hivyo, kufuatia sakata la mamlaka ya mapato nchini TRA
kuchukua sehemu ya fedha za maandalizi za vilabu vya ligi kuu, kutokana na deni
la kodi ambayo ilistakiwa kupitia mishahara ya makocha wa timu za taifa.
Bonifas Wambura amesema licha ya
kauli ya kuanza kwa mzunguuko wa pili kusubiriwa, pia kamati ya ligi
inasubiriwa kutoa kauli ya kuendelea kwa liugi daraja la kwanza ambayo nayo
ilisimama.
0 comments:
Post a Comment