AYEW NJE MATAIFA YA AFRIKA



        
Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika kuanza nchini Afrika kusini kocha wa timu ya taifa ya Ghana Kwesi Appiah amemuondoa kikosini mchezaji Andre  ‘Dede’ Ayew kutokana na kuwa majeruhi.
Habari zilizopatikana hii leo imemkariri kocha huyo akisema amefikia uamuzi wa kumwacha mchezaji huyo baada ya kushindwa kujiunga na wenzake kambini huko Abu Dhabi kufuatia kutopona jeraha la misuli ya paja.
Mwisho wa kutaja vikosi kwa nchi zitakazoshiriki fainali za kombe la mataifa ya  Afrika mwaka huu ni january 9 na kutokana na Ayew anayeichezea Marseille ya Ufaransa kushindwa kupona vyema inamfanya ashindwe kujumuishwa kikosini.
Fainali za kombe la mataifa ya Afrika zinataraji kuanza januari 19 nchini Afrika Kusini na kufikia tamati yake mwezi february.

0 comments:

Post a Comment