PINDA AAHIDI KUKUZA KIKAPU NCHINI.




                
SERIKALI nchini imeahidi kuendelea kuunga mkono michezo nchini ikiwa ni pamoja na Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kukarabati miundombinu ya viwanja vya michezo.


Ameyasema hayo Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kanda ya tano ya mpira wa kikapu yaliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini huku ya kishirikisha jumla ya timu 13 kutroka katika nchi saba.

Amesema, Serikali itaendelea kuunga mkono kwa nguvu zake zote maendeleo ya michezo nchini hususani katika nyanja ya miundo mbinu ya viwanja.

"Nazungumza kama Serikali tutaendelea kuunga mkono kwa nguvu zetu zote maendeleo ya michezo Tanzania na ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki," alisema Pinda.

Aliongeza kuwa, Mpira wa kikapu ni mchezo wenye changamotokubwa kwa wachezaji kwa kuwa unahitaji kuwa na wachezaji wenye nguvu na afya kutoka na aina yenye ya mchezo na nimchezo unaotumia kiwanja kidogo hivyo kuwataka wachezaji kujituma katika kutoa ushindani wa kweli.

Waziri pia amesisitiza nidhamu miongoni mwa wachezaji wote wanaoshiriki mashindano ambayo ameyataja kuwa yanajenga uelewa na amani miongoni mwao.

Akizungumzia mashindano hayo Rais wa Shirikisho la Mpira wa kikapu Nchini (TBF) Musa Mziya ameiomba Serikali iangalie kwa macho mawili swala la miundombinu laviwanja vinavyokidhi hadhi ya mashindano makubwa kama hayo.

Amesema, mshindi wa mashindano haya atawakilisha nchi yake katika mashindano ya klabu bingwa Afrika yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Duniani (FIBA).

Pamoja na Pinda viongozi wengine walioudhuria mashindano hayo ni Waziri wa Habari Vijana, Utamaduni na Michezo Fenella Mukangara, Balozi wa Rwanda, Balozi wa Somalia, Naibu Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya michezo nchini, Juliana Yasoda .

Katika mechi ya awali kwa upande wa Wanawake timu ya Tanzania 'Tanzanite Queens' ilianza vibaya michuano hiyo kwa kufungwa kwa pointi 74 - 32 na timu ya Kenya katika mchezo ambao Tanzanite ilionekana kuzidiwa kila idara kutokana na wachezaji wa Kenya kuwa warefu.

Nchi zinazoshiriki katika mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Misri, Burundi na Somalia.

0 comments:

Post a Comment