
kabange siku ya mechi ya kirafiki na Tusker ya kenya mwishoni mwa mwaka jana.
Mchezaji Alain Kabange Twite
hataweza kuichezea Yanga msimu huu (2012/2013) baada ya klabu hiyo kuingiza
nyaraka zenye upungufu wakati ikimuombea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC)
kwa njia ya mtandao (Transfer Matching System- TMS).
Kwa mujibu wa Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), baadhi ya nyaraka zenye upungufu katika
maombi hayo ni mkataba kati ya Twite na Yanga, lakini vile vile makubaliano ya
mkopo (Loan Agreement) kati ya Yanga na FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo (DRC) ambayo ndiyo inayommiliki mchezaji huyo.
Ili mchezaji aweze kupata ITC kwa
njia ya TMS, kwa mujibu wa Kanuni za Uhamisho wa Wachezaji za TFF kuna nyaraka
kadhaa muhimu zinatakiwa kukamilika katika maombi hayo ili hati hiyo iweze kupatikana.
0 comments:
Post a Comment