Idadi ya wadau waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania uongozi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeongezeka ambapo wengine saba wamechukua leo (Januari 15 mwaka huu) na kufanya idadi yao kufikia 26.
Hata hivyo,
idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani
vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa
10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.
Waliochukua
leo ni Michael Wambura anayewania umakamu wa rais wakati kwa wajumbe wa Kamati
ya Utendaji ni Mbasha Matutu, Muhsin Balhabou, Salum Chama, Titus Osoro na
Zafarani Damoder.
Idadi kamili
ya waliochukua Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (Makamu wa
Rais). Kwa upande wa wajumbe na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera
na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano
(Mara na Mwanza).
Epaphra Swai
na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Twahili
Njoki (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo,
Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama
(Njombe na Ruvuma).
Athuman
Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida),
Farid Nahdi (Morogoro na Pwani), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na
Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es Salaam).
Naye Said
Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL
Board).
0 comments:
Post a Comment