NEWCASTLE WAFANYA MAKUBWA KWENYE USAJILI.



 
Klabu ya soka ya Newcastle United inayoshiriki ligi kuu ya England imethibitisha kumsajili aliyekuwa mchezaji wa timu ya Montpellier  ya Ufaransa Mapou Yanga-Mbiwa kwa mkataba wa miaka mitano na nusu.


Yanga-Mbiwa  ambaye alikuwa nahodha wa Montpellier amekabidhiwa jezi namba 13 na anatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza akiwa na Newcastle United jumanne ijayo dhidi ya Aston Villa.

Akizungumza mara baada ya kuthibitishwa rasmi  kuwa mchezaji wa Newcastle United Yanga-Mbiwa amesema anajisikia faraja kuitumikia timu hiyo huku kocha Alan Pardew akisifu kipaji kikubwa alichonacho nyota huyo.

Uongozi wa Montpellier  jana ulithibitisha kufikia makubaliano na Newcastle United juu ya uhamisho wa raia huyo wa Ufaransa  ambaye ameripotiwa kufaulu vipimo vya afya na kukubaliana mambo binafsi na timu yake mpya.

0 comments:

Post a Comment