KAMATI YA MUUNGANO KUZIBA PENGO LA MWENYEKITI.



Kamati ya kombe la Muungano ipo katika mikakati ya kujaza nafasi za uongozi wa kamati hiyo ikiwemo nafasi ya mwenyekiti iliyoachwa na mbunge wa zamani wa Mufindi Marehemu Benito Malangalila.
Mratibu wa mashindano hayo, Daudi Yassin amesema kukamilika kwa zoezi hilo litakalo chukua wiki mbili kutoka sasa litafanikisha zoezi la uandaaji wa michuano hiyo kwa mwaka huu.
Msimu uliopita michuano ya Muungano haikufanyika kutokana na kuchelewa kwa ukamilifu wa mipango ya udhamini unaofanikisha michuano hiyo kufanyika bara na visiwani.

0 comments:

Post a Comment